The House of Favourite Newspapers

Majeshi ya China na Urusi Yafanya Mazoezi ya Pamoja Yenye Lengo la Kuimarisha Uhusiano

0
Majeshi ya China na Urusi yanafanya mazoezi ya pamoja kuimarisha uhusiano

BEIJING na Moscow zina uhusiano wa karibu wa kiulinzi na China imesema inataka kusukuma uhusiano wa nchi hizo mbili “katika kiwango cha juu,” hata wakati Moscow inakabiliwa na vikwazo vya kimataifa na kulaaniwa kwa uvamizi wake wa Februari 24 nchini Ukraine.

Majeshi ya nchi zote mbili yanaendelea na mazoezi ya pamoja

“Lengo ni kuimarisha ushirikiano wa kivitendo na wa kirafiki na majeshi ya nchi zinazoshiriki, kuongeza kiwango cha ushirikiano wa kimkakati kati ya pande zinazoshiriki, na kuimarisha uwezo wa kukabiliana na vitisho mbalimbali vya usalama,” wizara ya ulinzi ya China ilisema katika taarifa yake.

 

India, Belarus, Mongolia, Tajikistan na nchi zingine pia zitashiriki, ilisema.

 

Uhusiano kati ya Urusi na China umekua ukikaribia zaidi chini ya Rais wa China Xi Jinping na mwenzake wa Urusi Vladimir Putin, na Beijing imekuwa chini ya shinikizo kwa upinzani wake kwa vikwazo vilivyowekwa na nchi nyingi za Magharibi juu ya vita. Muda mfupi kabla ya uvamizi huo, Moscow na Beijing zilikubaliana juu ya ushirikiano wa “bila kikomo”.

Makamanda wa Urusi na China wakisalimiana

Beijing ilisema uamuzi wake wa kushiriki katika mazoezi ya pamoja “hauhusiani na hali ya sasa ya kimataifa na kikanda”.

 

Mazoezi hayo ya Vostok ni mazoezi ya pili ya pamoja ya kijeshi yaliyofanywa na wanajeshi wa China na Urusi mwaka huu.

 

Imeandikwa: Peter Nnally kwa msaada wa mitandao

Leave A Reply