Majeshi ya Israel Yashambulia Waombolezaji Kwenye Mazishi ya Shireen Abu Akleh

 

Waombolezaji wakiomboleza kifo cha  Shireen Abu Akleh

MAZISHI yanafanyika leo ya mwandishi wa habari Shireen Abu Akleh aliyeuawa na majeshi ya Israel nchini Palestina katika kambi ya wakimbizi ya Jenin ambako alikuwa akiripoti matukio ya ukatili na unyanyasaji wa wanajeshi wa Israel ambako alipigwa risasi ya kichwa na kufariki dunia.

 

Katika hali isiyokuwa ya kawaida wanajeshi wa Israel wameingilia kati na kuwashambulia waombolezaji wakiwalazimisha kutaka kuuchukua mwili wa marehemu Shireen wakati wanauondoa katika hospitali ya Kifaransa ya St. Louis.

 

Mwandishi wa Al- Jazeera Marwan Bishara amesema:

 

“Kwanini jambo hilo lihitaji aina ya vurugu kiasi hiki.”

 

Naye Imran Khan ripota wa Al-Jazeera kutoka mashariki mwa Jerusalem amesema:

wanajeshi wa Israel wakiwazuia raia wa Palestina kuubeba mwili wa Shireen Abu Akleh

“Kilichotokea ni mvurugano na msukumano baina ya majeshi ya Israel na waombolezaji ambao walikuwa wanataka kubeba mwili wa Shireen kanisani, waombolezaji walitaka kutembea na mwili wake hawakutaka ubebwe na gari.”

Kwa mujibu wa taarifa kutoka Wizara ya habari ya Palestina inadai jumla ya waandishi wa habari 45 wameshauawa kwenye na majeshi ya Israel tangu mwaka 2000.706
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment