The House of Favourite Newspapers

MAJESHI YA TANZANIA NA MSUMBIJI YAUNGANA KULINDA AMANI

Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Simon Sirro (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari leo.
Viongozi hao wakisaini makubaliano ya kushirikiana katika kupambana na uhalifu baini ya nchi hizo mbili.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Tanzania, Simon Sirro na Mkuu wa Jeshi la Polisi Msumbiji, Bernadino Rafael,(kushoto)  wakionyesha mikataba ya makubaliano.

MKUU wa Jeshi la Polisi Tanzania, Simon Sirro na Mkuu wa Jeshi la Polisi Msumbiji, Bernadino Rafael, leo Jumatatu wametiliana saini ya makubaliano ya kushirikiana katika kupambana na uhalifu baini ya nchi hizo mbili.

 

Akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam, Sirro amesema kuwa ushirikiano huo utaleta tija baina ya nchi hizo mbili kwani kumekuwa na wimbi la uhalifu nchini Msumbiji ambapo wahalifu hao hukimbilia Tanzania au wahalifu wa Tanzania kukimbilia Msumbiji.

 

Siro ameongeza kuwa katika matukio ya huko nyuma ambayo yalikuwa yakifanywa na vikundi vya kigaidi wilayani Rufiji mkoani Pwani, wameshabaini wahalifu hao walikimbilia Msumbiji ambapo hivi sasa jeshi la polisi limejiimarisha vilivyo kuhakikisha linawakamata wahalifu hao popote walipokimbilia.

Kwa upande wake Mkuu  wa Jeshi la Polisi  kutoka Msumbiji, Bernadino Rafael  amesema kuwa wamefanya makubaliano hayo ili kudhibiti matukio ya kihalifu hasa ya kuimalisha zaidi ulinzi kwenye mipaka ili waweze kuwakamata kiurahisi  wahalifu wanaotenda makosa na kukimbilia nchi jirani.

Comments are closed.