The House of Favourite Newspapers
gunners X

Majibu ya Nenga kwa Nandy Yashtua

0

NANDY au The African Princess ni malkia wa muziki Afrika Mashariki akiwa ni zao la Nyumba ya Kukuza Vipaji
Tanzania (THT).


Ni mwimbaji, mwandishi wa
nyimbo, balozi wa brandi mbalimbali, mfanyabiashara na ni mchumba wa Rapa
wa Bongo, Billnass au Nenga.
Nandy anasema anampenda Nenga pamoja na kwamba aliwahi kumsaliti na
kwenda kupata mtoto na mwanamke
mwingine.


Katika moja ya posti zake wikiendi
iliyopita, Nandy aliwauliza wafuasi wake swali akitaka kujua wanataka kuona nini
kutoka kwake kwa mwaka 2022 ndipo
Nenga amekuja kutoa majibu ya kushtua baadhi ya watu.


Nenga amemjibu Nandy kwamba,
angependa kumuona akipigana na mke mwenzie; majibu ambayo yametafsiriwa kuwa huwenda anamsaliti. Nandy ameuliza; “Eti mwaka huu unatamani kuona nini kutoka kwangu?”
Ndipo Nenga akamjibu; “Ukipigana na
mke mwenzio…”


Hata hivyo, Nandy hakujibu kuonesha
kwamba hakupendezwa na komenti hiyo. Kwa sasa wawili hao wamekuwa
wakijinasibu kwamba wapo kwenye mahaba
motomoto huku wakiapa kufunga ndoa mwaka huu; jibu ambalo ndilo alilotaka kulisikia Nandy.

Leave A Reply