The House of Favourite Newspapers

Majimaji Yaanika Kilichowaponza Kwa Ruvu

0

BAADA ya juzi Jumamosi Majimaji FC kupoteza mechi yake dhidi ya Ruvu Shooting, kocha mkuu wa timu hiyo, Peter Mhina, ameweka bayana sababu kuu zilizowafanya kupata matokeo hayo.

Majimaji inayodhaminiwa na Kampuni ya Kubashiri Matokeo ya Sokabet, juzi Jumamo­si ilipoteza mechi hiyo kwa mabao 2-1 katika Uwanja wa Mabatini, Pwani.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Mhi­na alisema: “Hakuna kingine kilichosababi­sha tufungwe zaidi ya hali ya hewa ya Pwani ilivyo tofauti na kwetu Songea.

“Tumekutana na hali ya hewa ya joto sana hali ambayo iliwafanya wachezaji wangu kushindwa kucheza vizuri na kujikuta tuki­fungwa kirahisi.”

Omary Mdose | Dar es Salaam | Championi.

Usipitwe na Matukio, Install App Yako ya Kijanja na Namba Moja Tanzania ya Global Publishers

Android ===>Google Play

iOS ===>Apple Store

 

Leave A Reply