The House of Favourite Newspapers

Majina 31 Wachezaji wa Simba Yaliyotumwa CAF

0

KLABU ya Simba SC imewasilisha majina ya wachezaji 31 waliosajiliwa kwaajili ya Ligi ya Mabingwa Barani Afrika msimu wa 2021/2022 imeelezwa.

 

Klabu hiyo itakayoiwakilisha Tanzania kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika imepeleka idadi kubwa ya wachezaji waliosajiliwa CAF kwa mara ya kwanza tangu ilipoanza kushiriki michuano hiyo.

 

Kwa upande wa watani zao Yanga SC, imeelezwa kuwa wao wamewasilisha orodha ya wachezaji 28 waliowasajili kwaajili ya michuano hiyo ya Klabu Bingwa Afrika.

 

Wachezaji hao waliosajiliwa kwaajili ya michuano ya Afrika, upande wa walinda lango wapo wanne (4) ambao ni; Aishi Salum Manula, Benno David Kakolanya, Jeremiah Kisubi na Ally Salim.

 

Mabeki ni tisa (9) ambao ni; Erasto Edward Nyoni, nahodha msaidizi Mohammed Hussein Tshabalala, Gadiel Michael, Henock Inonga ‘Varane’, Israel Mwenda, Joash Onyango, Pascal Wawa, Kennedy Juma na Shomari Salum Kapombe.

 

Viungo wapo kumi na tatu (13) ambao ni; Abdulswamad Kassim, Bernard Morrison, Duncan Nyoni, Hassan Dilunga, Jimmyson Mwanuke, Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Pape Ousmane Sakho, Peter Banda, Rally Bwalya, Sadio Kanoute, Thadeo Lwanga na Ibrahim Ajibu Migomba.

 

Washambuliaji wenyewe wapo watano (5) ambao ni; Nahodha John Raphael Bocco, Meddie Kagere, Chriss Mugalu, Yusuph Mhilu na Kibu Denis.

Leave A Reply