Majizzo na Lulu Hakuna Dalili ya Ndoa

 

MCHUMBA wa staa wa Bongo Movie Elizabeth MichaelLulu’, Francis SizaDj Majizzo’ ameonesha kumkubali Mrembo huyo kwa uvumilivu wake kipindi chote tangu amvishe Pete mwanzo mwa mwaka huu na kuhudhuriwa na watu lukuki akiwemo rafiki yake wa karibu Dk. Cheni.

 

Kupitia ukurasa wa mtandao wa kijamii wa Instagram wa Majizzo ameandika ujumbe kama ishara ya kuonyesha kumkubali Lulu.

“Nakukubali mshikaji wangu japo mwaka umeisha na ndoa haina dalili lakini bado hujanikatia tamaa nakukubali Sana.”

 

 

Aidha, Mrembo huyo wa tasnia ya Bongomovie hakusita kumjibu mchumba wake; “Nakukubali bro, Mswahili Numero uno tushakuwa ndugu tena maana umenipiga password mpaka tumeanza kufanana yote kheri 2019 nimekosa wedding nimepata twin.”

 

Hata hivyo Majizzo amempongeza mwanadada Maua sama kwa kuingia jukwaani kwa aina yake akiwa juu ya chuma na kulitendea haki jukwaa la tamasha Muziki mnene lililofanyika wiki iliyopita katika viwanja vya Tanganyika Packers kawe jijini Dar es salaam.

 

“Waswahili tulikua na hofu kama umeweza kupanda kwenye stage ukiwa juu ya hilo chuma,haikuwa ngumu kwako ukatimiza majukumu yako.”

 

Toa comment