MAJONZI: Babu Tale AISHIWA NGUVU, Mwili wa Mkewe Ukitolewa Ndani -Video
Mwili wa Shamsa Kombo aliyekuwa Mke wa meneja wa WCB, Hamis Taletale maarufu kama Bubu Tale anatarajiwa kuzikwa leo mkoani Morogoro. Shamsa alifariki dunia siku ya jumapili tarehe 28, Juni 2020 baada ya kuugua na kulazwa.
Msiba huo umewagusa sana wadau wa burudani hapa Tanzania, wasanii, wadau wa habari na watu wengi maarufu wameonekana msibani na kueleza ni namna gani wameguswa na msiba huo.
Msafara kwa ajili ya kwenda kumpumzisha Shamsa umeondoka leo jijini Dar es salaam kuelekea kijiji cha mkuyuni mkoani Morogoro kwa ajili ya maziko yatakayofanyika leo tarehe 29, June 2020.