The House of Favourite Newspapers

MAJONZI! SALA ALIVYOTUMBUKIA NA NDEGE YAKE KWENYE BWAWA LA KEMIKALI!

NI majanga! Inaelezwa kuwa ndege iliyopotea na straika matata Emiliano Sala inawezekana isipatikane tena baada ya kuzama ndani ya maji kwenye bonde lenye urefu wa futi 600.

Bonde hilo li­lilopo katika visi­wa vya Alderney, Uingereza, lilitu­mika kwa watu kumwaga kemikali za silaha zilizotu­mika kwenye Vita ya Kwanza ya Dunia, pamoja na takataka ny­ingine za tani 17,000.

Imeelezwa kuwa ni ngumu kwa ndege hiyo kupatikana kutokana na kuzama katikati ya kemikali na takataka hizo, na hivyo kuchanganyikana, tena ukiwa ni umbali mrefu kwenda chini.

 

Hili linakuja baada ya rubani ambaye alikuwa na Emiliano kwenye ndege hiyo, kudaiwa kuwa hana leseni ya biashara na alikuwa na deni la pauni 18,000 (Sh mil 55).

Emiliano alipotea na ndege akiwa yeye na rubani alipokuwa akitokea Ufaransa kwenye kla­bu yake ya Nantes na kwenda Cardiff City England ambako al ikuwa ‘ ames­inya’ (amesaini) mkataba.

LONDON, England.

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.