The House of Favourite Newspapers

Yafahamu Makabila 10 Maarufu Zaidi Barani Afrika

 

WATU wa nje ya Afrika hufikiri watu wa bara hili ni mkusanyiko wa jamii moja inayoelewana kwa lugha na kiutamaduni, kumbe sivyo.  Kuna makabila zaidi ya 3,000 yenye kujitegemea katika kila fani.  Miongoni mwa makabila kumi makubwa na maarufu ni yafuatayo:

1. Wazulu
Ndilo kabila kubwa zaidi Afrika Kusini likiwa na watu wapatao milioni 11 na huenda likiwa ndilo maarufu zaidi Afrika ambapo hata watalii wengi wa nje hupenda kuelewa zaidi kuhusu kabila hilo ambalo miongoni mwa viongozi wake wa jadi  alikuwa Shaka.

2. Wamaasai
Maasai ni kabila maarufu Kenya na Tanzania likiwa na utamaduni wao wa kipekee Afrika na likijulikana zaidi kwa ufugaji hususan ng’ombe.

3. Waoromo
Ni kabila maarufu na kubwa zaidi Ethiopia, likifanyiza asilimia 35 ya idadi ya watu nchini humo.  Pia liko kaskazini mwa Kenya na sehemu za Somalia.

4. Wayoruba
Idadi yao ni milioni 35.  Wengi wao huishi Nigeria, wengine kusini mwa Benin.  Ndilo kabila kubwa zaidi Afrika.

5. Wakalenjin

Kabila hili ambalo hupatikana Kenya ndilo maarufu zaidi kwa wanariadha wa mbio ndefu duniani.

6. Wahausa 

 Ni kabila kubwa linalopatikana katika nchi za Sudan, Niger, Nigeria, Chad, Togo, Cote d’Ivoire, Sudan na Ghana.

7. Wahimba

Hawa ni moja ya makabila maarufu Afrika; ni wakazi wa Namibia, maarufu kwa ‘kujipodoa’ miili yao kwa udongo mwekundu hivyo kujulikana kama “watu wekundu”.

8. San Bushmen

Kabila ambalo kwa Kiingereza wanajulikana kama San Bushmen, liko magharibi mwa Botswana ambapo ni maarufu kwa filamu ya The Gods Must Be Crazy waliyoshiriki kuicheza.  Wanaishi katika sehemu zenye ukame mkubwa wa maji.

9. Wachagga

Hawa huishi katika miteremko ya Mlima Kilimanjaro nchini Tanzania, wakiaminika kuwa Waarika wa kwanza kufuata Ukristo, jambo lililowafanya kupata elimu na maisha bora zaidi miongoni mwa nchi zilizokuwa makoloni barani Afrika.

 

10. Wa-Xhosa  

Hawa wanaishi Afrika Kusini na ni maarufu kutokana na  mtindo wao wa kipekee wa kuzungumza, hususani kwa kuchezesha ulimi mdomoni.

 

 

 

Comments are closed.