The House of Favourite Newspapers

Makalla Achangisha Zaidi ya 1.5M za Matibabu ya Mwenezi wa Chadema

CHAMA Cha Mapinduzi Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa kimechangia kiasi cha Sh 1,553, 500 kwa ajili ya Katibu Mwenezi wa Baraza la Wanawake wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Sigrada Mligo kwa ajili ya kwenda kupata matibabu katika hospitali ya Peramiho.

Katibu wa Halmashauri Kuu (NEC), Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa, CPA Amos Makalla amepitisha harambee hiyo leo wakati akizungumza na wananchi katika Uwanja wa Mashujaa Wilaya ya Mafundi mkoani Iringa ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya siku tatu katika mikoa ya Mbeya na Iringa.

Awali, Makalla amesema kuwa jana akiwa katika mkoa wa Mbeya alitoa pole kwa Sigrada na kukitaka chama chake katika mkoa wa Njombe kwenda kumtembelea na kumpa salamu na pole na aliweza kuongea naye kwa simu na kumpa pole.

Amesema wakati akizungumza naye alisema anatakiwa kwenda kufanya matibabu katika hospital ya Peramiho na kusema kuwa yeye alimuwezesha lakini Sigrada anahitaji msaada ili aweze kujiuguza na kutibiwa na kuweza kurudi katika hali yake ya kawaida.

“Sigrada anahitaji msaada na mimi kama mwenezi wa Chama Cha Mapinduzi lazima wenezi tusaidiane na mimi nawaomba hapa tuanzishe mchango wa kumchangia Sigrada kwa ajili ya matibabu yake aendelee kujiuguza ameniambia anaenda karantini nimemuwezesha lakini lazima tuendelee kumchangia,” amesema Sigrada.

Katika harambee hiyo Mjumbe wa Halmashauri Kuu wa CCM Mkoa wa Iringa, Asas Abri amechangia kiasi cha Sh milioni moja na Sh 553,500 zilipatikana kutokana na michango iliyotolewa na wana CCM katika Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.