The House of Favourite Newspapers

Makalla Ampigia Simu Live Waziri wa Fedha Kujua Fidia za Wananchi Kipunguni

 “Wakati namsikiliza Mbunge wenu Mhe Bonna ameeleza kwa Uchungu na masikitiko Kwamba kuna Wananchi wanadai fidia na wameahidiwa kulipwa lakini bado hawajalipwa mpaka Sasa Wananchi wa Kipunguni na bahati nzuri Dkt Samia suluhu Hassan anajeshi zuri la Mawaziri na Muda wote wako tayari kutatua kero na hili nampigia Mhe Waziri wa Fedha Mhe Mwigulu Lameck Nchemba atupe Majibu vipi wanalipwa lini Fidia zao.
Nae Mhe Waziri Dkt Mwigulu Lameck Nchemba amekiri kufahamu jambo hilo na hata yeye amezungumza sana Mhe Mbunge wa Segerea na kweli waliahidi kulipa ila kulingana na kuingiliana kwa mambo ya kiserikali wamechelewa kulipa ila wanatoa ahadi kwamba kuanzia Mwezi wa Nane Wananchi wa Kipunguni wanataanza kulipwa Fedha zao.
Pia Katibu wa NEC Itikadi Uenezi na Mafunzo CPA Makalla amesema katika Mkutano huo fedha zikianza kulipwa aitwe nae ashuhudie  pamoja na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam ili kuwadhibitishia Wananchi kuwa Serikali ya Dkt Samia ikiahidi inatekeleza.