The House of Favourite Newspapers

Makalla Asafiri na Treni ya SGR Kutoka Morogoro Kwenda Dar, Ampongeza Rais Samia Kwa Kazi Kubwa..

Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mafunzo wa CCM Taifa CPA Amos Makalla amesafiri na Treni Mpya ya Mwendokasi (SGR) kutoka Morogoro mpaka Dar es salaam.
Mwenezi Makalla amesema amefurahi kuwa miongoni mwa abiria waliosafiri na treni ya SGR kutoka Morogoro mpaka Dar es salaam na kuongeza kuwa ni Treni nzuri yenye huduma nzuri na haichoshi.
” Mimi nakumbuka nilikuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam wakati Mhe Samia suluhu Hassan anachukua Urais kipande hiki cha Dar es salaam Morogoro kwa wakati ule kilikuwa asilimia 42 lakini amefanya kazi kubwa na kwasasa kimekamilika  na wakati wote naambiwa itazinduliwa safari za Dar es salaam mpaka Dodoma” Mwenezi Makalla.