Kartra

Makalla Kuwakabidhi Kombe Simba Uwanja wa Mkapa

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Amos Makalla anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mchezo wa Simba dhidi ya Namungo FC utakaopigwa kesho kwenye Uwanja wa Benjamini Mkapa jijini Dar es Salaam.

Baada ya kumalizika kwa mchezo huo uliopangwa kuanza 10:00 jioni, itafanyika sherehe fupi ya kukabidhi Ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom 2020/2021 zoezi ambalo linatarajiwa kuongozwa na Makalla.

Simba walitwaa ubingwa wa Ligi Kuu Julai 11 baada kufikisha alama 79 kufuatia ushindi wa mabao 2-0 walioupata dhidi ya Coastal Union FC kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa na kujihakikishia alama hizo ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote.


Toa comment