Makalla: Miaka 48 ya CCM Imeleta Mapinduzi Makubwa katika Jamii

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimesema kina mengi ya kujivunia katika kuadhimisha miaka 48 ya chama hicho, kwani kimeendelea kuleta mapinduzi na mageuzi makubwa kiuchumi na kijamii kwa kuleta maendeleo sekta mbalimbali.
Katibu wa NEC, Itikadi, Ueneza na Mafunzo wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), CPA Amos Makalla ameeleza hayo leo Februari 2,2025 wakati akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es salaam ikiwa ni shamrashamra za kuelekea kilele cha maadhimisho ya miaka 48 ya CCM yanayotarajiwa kufanyika Februari 5, mwaka huu jijini Dodoma ambapo Mgeni Rasmi ni Mwenyekiti Taifa wa Chama cha Mapinduzi Dkt. Samia Suluhu Hassan.
Makalla amesema kuwa wakati chama hicho kikiadhimisha miaka 48 tangu kuanzishwa kwake kinakwenda sambamba na mambo ambayo yameweza kufanyika tangu kuzaliwa kwake.