The House of Favourite Newspapers

Makamba: Kuanzia Machi 2, Ukikutwa na Viroba Utakiona

SERIKALI kupitia Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira imesema kuwa tamko lililotolewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alivyoagiza kuondoa pombe zote zilizopo kwenye vifungashio vya karatasi (viroba), ametoa onyo kuwa atakayeendelea kuvisambaza mitaani atachukuliwa hatua kali kuanzia kesho.                        

Akizungumza na wanahabari jijini Dar es Salaam leo, waziri mwenye dhamana ya wizara hiyo, Januari Makamba amesema kuwa oparesheni juu ya katazo hilo itazingatia ibara ya 8(1) b na 14  sheria ya mazingira ya mwaka 2014 na kanuni zake.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Januari Makamba akizungumza na wanahabari. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Prof. Faustine Kamuzora.

Makamba ameeleza kuwa Oparesheni ya Kukagua Utekelezaji wa Agizo la Serikali la Usitishaji, Utengenezaji, Uuzaji na Matumizi ya Pombe zinazofungashwa kwenye vifungashio vya plastiki itaendeshwa nchini kote kuanzia Machi 2, 2017 kupitia kamati za ulinzi na usalama na kamati za mazingira katika ngazi ya mikoa, wilaya, tarafa, kata na vijiji.

“Kama tangazo letu la Februari 20, 2017 lilivyoonesha muda wa nyongeza unaweza kutolewa kwa wazalishaji halali ambao wataonesha ushahidi wa kuelekea kuhamia kwenye teknolojia ya chupa.

“Watahitaji muda mfupi kufanya hivyo na ambao watatimiza  masharti kadhaa na kupata kibali maalum kabla ya tarehe 28, Februari mwaka huu lakini wapo watu tisa ambao tayari wameleta maombi na tutaangalia kama wamekidhi vigezo au la.” alisema Makamba.

NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

Comments are closed.