Makambo Atawafunga Sana

 

Straika wa Yanga mwenye mabao 11, Heritier Makambo

KOCHA wa Yanga, Mwinyi Zahera amesema straika wake mwenye mabao 11, Heritier Makambo atatupia sana mzunguko wa pili kama hatajichanganya. Kwa sasa Yanga ipo kwenye nafasi ya kwanza katika msimamo wa ligi, ikiwa imejikusanyia pointi 50 katika michezo 18 iliyocheza.

 

Akizungumza na Spoti Xtra linalotoka kila Alhamisi na Jumapili, Zahera alisema; “Nadhani watu wanatakiwa kuangalia na si kubeza kabla hawajaona uwezo wa mtu, mimi namjua sana Makambo ni mchezaji anayejua sana kufumania nyavu.” “Utaona leo hii kila mmoja anamsifi a lakini kipindi tunaanza ligi walianza kumlaumu pamoja na kwamba mimi nilikuwa nikiwaambia ni mzuri kwa kufunga.

 

“Kama Makambo ataachana kabisa na mambo ya anasa za hapa nchini, basi atakuja kufunga mabao mengi ambayo yatamshangaza kila mtu kwani mimi najua uwezo wake.

 

“Mzunguko wa pili kama Mungu atamjalia uzima basi mimi naona kama anaweza kabisa kufi kisha hata mabao zaidi ya ishirini kwani hata mwanzo asingeyumba na mambo ya mjini leo hii angekuwa ana zaidi ya mabao hayo 11,” alisema Zahera

MUSA MATEJA, DAR ES SALAAM

Loading...

Toa comment