The House of Favourite Newspapers

Makambo Aweka Rekodi, Mayele Ampa Tano

0

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Heritier Makambo, ameweka rekodi kwenye mashindano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kufunga kwenye mechi mbili mfululizo.


Kwenye mechi hizo mbili
ambazo ni sawa na dakika 180, Makambo amefanikiwa kufunga mabao mawili na
yote ni kipindi cha kwanza.


Alianza mbele ya Taifa
Jang’ombe akifunga bao la kuongoza dakika ya 32, mchezo huo Yanga ilishinda
kwa mabao 2-0. Bao la pili
lilifungwa na Denis Nkane.

 

Mchezo wa pili mbele ya KMKM kwenye sare ya 2-2 ambapo, Makambo alipachika bao dakika ya 45, bao la pili lilifungwa na Feisal Salum.


Makambo amewapoteza
pia mastaa wa Simba kwa kuwa hakuna mwenye mabao zaidi ya mawili katika
mechi mbili walizocheza
na ni Pape Sakho na Rally Bwalya hawa wametupia bao mojamoja kwa upande wa Simba.


Wakati Makambo akifanya
hivyo, mshambuliaji mwenzake wa Yanga, Fiston Mayele, ameibuka na kukisifia kiwango cha mshambuliaji huyo ambacho amekionesha kwenye michuano ya Mapinduzi.

 

“Pongezi kwa Makambo na timu yangu kwa ujumla wamepambana mpaka kufika katika hatua kubwa ya michuano hii.

 

Kwa Makambo pia ni jambo zuri kuisaidia timu, amefunga katika kichezo yote miwili na hii itamfanya kuzidi kufanya vizuri katika michezo ijayo.

 

“Ukiwa kama mshambuliaji furaha kubwa inakuja pale ambapo utakuwa unafunga mabao ya kutosha, hivyo hata mimi naamini kuwa Makambo ana furaha kuona anafunga mabao kama mimi ambavyo nikifunga huwa nakuwa na furaha.”

STORI: LUNYAMADZO MLYUKA NA MARCO MZUMBE

Leave A Reply