Makambo, Mayele Waaga Ishu Ya Kutua Yanga

RASMI sasa hivi mshambuliaji wa AS Vita, Fiston Mayele na Heritier Makambo anayekipiga Horoya AC wanatua Yanga ni baada ya nyota hao kuwaaga mashabiki wa klabu zao.

Awali zilikuwa tetesi pekee, lakini hivi sasa rasmi nyota wanakuja Yanga baada ya kufikia muafaka mzuri wa kuja kukipiga Jangwani katika msimu ujao.

 

Yanga wanawasajili washambuliaji hao kwa ajili ya kuiimarisha safu yao ya ushambuliaji watakaokuja kuchukua nafasi za Fiston Abdulrazack na Michael Sarpong.

 

Kwa kupitia ukurasa wa kijamii wa Horoya, uliweka picha na ujumbe na picha ya kumuaga Makambo uliosomeka hivi: “Misimu miwili baada ya kuwasili kwako, sisi kama klabu tumemaliza ushirikiano.

“Tunakushukuru kwa utumishi wako mwaminifu, weledi wako na tunakutakia kila la kheri katika kazi yako yote. Asante.”

 

Hiyo ni ishara tosha kuwa mshambuliaji huyo anakuja kukipiga Yanga, hivi karibuni gazeti hili liliandika taaraifa za Makambo kuandika barua ya kusitisha mkataba wake wa mwaka mmoja alioubakisha kwa ajili ya kwenda kutafuta changamoto nyingine kwingine na ndiyo kilichotokea nyota huyo mkataba wake umevunjwa baada ya makubaliano ya pande mbili mchezaji na klabu.

 

Hiyo imejitokeza kwa Mayele ambaye yeye aliwaaga viongozi na mashabiki wa AS Vita kwa kupitia ukurasa wake wa mtandao ya kijamii kwa kusema kuwa: “Niwashukuru mashabiki wa AS Vita kwa kuwepo hapa kwa kipindi chote, nakwenda kutafuta changamoto nyingine kwingine.

 

Taarifa za kuaminika kutoka ndani ya klabu ya Yanga zinaeleza kuwa, Mayele na Makambo muda wowote watatua nchini kwa ajili ya kuwahi maandalizi ya msimu mpya ambao watashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika inayotarajiwa kuanza mwezi Septemba.

Stori: WILBERT MOLANDI NA MUSA MATEJA, Dar3403
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment