The House of Favourite Newspapers

Makambo: Tutaivua Simba Ubingwa

0

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Heritier Makambo, amefunguka kuwa baada ya kufanikiwa kuwavua Simba ubingwa wa Ngao ya Jamii, sasa mipango yao ni kuhakikisha wanawavua tena ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

 

Jumamosi iliyopita katika mchezo wa Kariakoo Dabi kuwania Ngao ya Jamii uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Dar, Yanga waliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Simba. Taji hilo lilikuwa likishikiliwa na Simba.

 

Akizungumza na Spoti Xtra, Makambo alisema: “Kwanza kabisa kama wachezaji tumefurahishwa sana na matokeo ya mchezo wetu dhidi ya Simba, ushindi lilikuwa jambo muhimu kwa kuwa tulikuwa tumetoka kutolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.

 

“Jambo zuri ni kuwa tumeshinda ubingwa wetu wa kwanza na sasa macho yetu yote ni kuhakikisha tunaanza vizuri mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Kagera Sugar, kama sehemu ya hatua za kutimiza lengo letu la kuwavua ubingwa wa Ligi Kuu Simba.

 

“Nina furaha kuwa tumeanza vizuri kwa kuwafunga watani wetu, kwetu huu ni mwanzo mzuri na nina imani tutazidi kufanya vizuri, huu ni mwaka wetu, tunawaahidi mashabiki kupambana kwa ajili yao.”

 

Ikumbukwe kuwa, Simba ndiyo mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara wakibeba ubingwa huo mara nne mfululizo kuanzia msimu wa 2017/2018 hadi 2020/21.

~~JOEL THOMAS NA CAREEN OSCAR, Dar

Leave A Reply