Makamu wa Rais Aifariji Familia ya Marehemu, Dkt. Faustine Ndugulile
Makamu Dkt. Philip Mpango, akisalimiana na ndugu, jamaa na marafiki waliojitokeza nyumbani kwa marehemu.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango ameifariji familia ya marehemu, Dkt. Faustine Ndugulile aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Kigamboni na Mkurugenzi Mteule wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kanda ya Afrika, nyumbani kwake Kigamboni Jijini Dar es Salaam leo tarehe 30 Novemba, 2024. Dkt. Ndugulile alifariki dunia tarehe 27 Novemba, 2024 nchini India alipokuwa akipatiwa matibabu.