The House of Favourite Newspapers

Makamu Wa Rais Aongoza Upandaji Miti Dar

makonda-mti-3-001Makamu wa Rais, Samia Suluhu akipanda mti aina ya Royal Palm katika kampeni hiyo ya kupanda mti katika Mkoa wa Dar es Salaam.makonda-mti-4-001…akiusimika vizuri katika shimo.

makonda-mti-6-001…akiusimika vizuri katika shimo.Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akipanda mti katika kampeni hiyo.makonda-mti-7….Makonda akimwagilia mti maji baada ya kuupanda.

makonda-mti-8-001Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum akipanda mti katika barabara ya Kilwa eneo la JKT Mgulani.

makonda-mti-1-001   Miongoni mwa viongozi mbalimbali waliofika katika kampeni hiyo wakiendelea na zoezi la kupanda mti na kumwagilia     makonda-mti-9-001Balozi wa Parestina Nchini Tanzania, Hazem Shabati akipanda mti wa aina ya Royal Palm katika kampeni hiyo.

makonda-mti-10-001Baadhi ya askali polisi nao wakishiriki zoezi la upandaji miti.

makonda-mti-11-001…Zoezi likiendelea.

makonda-mti-12-001Mmoja wa wananchi naye akishiriki zoezi hilo la upandaji miti aina ya Royal Palm.

 

makonda-mti-13-001Askari polisi wakiendelea na zoezi la kupanda miti.

makonda-mti-15-001Makamu wa Rais, Samia Suluhu akizungumza jambo katika hafla hiyo.

makonda-mti-14-001Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza jambo katika hafla hiyo.

makonda-mti-2-001Makamu wa Rais, Samia Suluhu (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na wadau wa zoezi hilo.

makonda-mti-16-001Baadhi ya wananchi waliofika katika zoezi hilo la upandaji miti katika Wilaya ya Temeke.

MAKAMU wa Rais, Samia Hassan Suluhu leo ameongoza wakazi wa Jiji la Dar es Salaam katika zoezi la Kampeni ya Upandaji Miti kwa  Mkoa wa Dar es Salaam lililofanyika katika Barabara ya Kilwa, jirani na Kambi ya JKT Mgulani.

Akizungumza na katika hafla hiyo, Samia Suluhu alisema anampongeza Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda kwa kuwa na dhamira ya kuwahamasisha wakazi wa jiji kupanda mti ili kuweza kuwa na jiji safi na lenye kuwa na upepo mzuri kila mahali.

Alisema zoezi hilo lisiwe katika jiji la Dar pekee bali liwe katika nchi nzima kwani uwepo wa miti katika maeneo mbalimbali unachangia kuwa na mazingira bora na kuondokana na majangwa ili hata vizazi vijavyo viweze kujua umuhimu wa kuhifadhi mazingira.

Naye Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda alisema kwa upande wa madereva wanaogonga kingo za vyuma vilivyowekwa pembezoni mwa barabara, ni lazima wachukuliwe hatua kali.

Aliwataka wanaohusika na suala zima la kuangalia mazingira hasa viongozi wa manispaa zote jijini kuwachukulia hatua kali watakaogonga kingo za vyuma, akasema warudishie mara mbili ya idadi ya vyuma ambavyo wamevigonga kwani karibu maeneo mengi ya jiji wamezungushia vyuma kwa ajili ya kulipendezesha jiji.

Na Denis Mtima/GPL.

Comments are closed.