Makamu wa Rais aongoza usafi Kinondoni

Mama Samia usafi (1)

Makamu wa Rais, Samia Suluhu (kulia) akifafanuliwa jambo na Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda.

Mama Samia usafi (2)

Akiweka takataka kwenye toroli.

Mama Samia usafi (3)

Wasanii nao wakifanya usafi.

Mama Samia usafi (4)

Kazi na dawa, hapa wasanii ‘wakijiselfisha’.

Mama Samia usafi (5)

Msanii wa filamu, Wastara, akiwa amebebwa kwenye toroli

IKIWA leo ni siku ya kuadhimisha miaka 54 ya Uhuru wa Tanzania Bara, ambapo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli, alitangaza kuwa ni siku maalum kwa ajili ya kufanya usafi, Makamu wa Rais, Samia Suluhu amewaongoza mastaa na watu mbalimbali kufanya usafi, Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kufanya usafi ulioanzia maeneo ya Morocco hadi Kinondoni B, Samia aliwataka wakurugenzi na wakuu wa mikoa kuyadhibiti makampuni yanayofanya tenda za usafi kwani wanakula fedha za serikali lakini jiji linaendelea kuwa chafu, jambo ambalo ni matumizi mabaya ya fedha za wananchi.

“Nawapongeza sana wasanii na watu mbalimbali mliojitokeza kufanya usafi, zoezi hili liwe endelevu, viongozi watenge siku maalumu za kufanya usafi ili jiji letu liwe safi, pia kuna makampuni ambayo yanachukua tenda za usafi lakini hayafanyi kazi ipasavyo, tunahitaji taarifa za hayo makampuni kwani fedha za serikali zinatumika ndivyo-sivyo,” alisema.

Picha/stori: Gladness Mallya/GPL

Loading...

Toa comment