Makamu wa Rais Awasili Arusha kuwa Mgeni Rasmi Kongamano la Nne la Uhuru

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango amewasili mkoani Arusha na kupokelewa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Paul Christian Makonda kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro mapema leo Septemba 20, 2024.
Dkt Mpangoa anatarajiwa kuwa Mgeni Rasmi katika Kuhitimisha Kongamano la 4 la Uhuru wa Kidini la Afrika litakayofanyika katika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha Septemba 21, 2024.
