Samia Azindua Radio Jamii, Ukatili Dhidi ya Wanawake
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, leo Agosti 12,2020, amezindua rasmi Kituo cha Redio Jamii Kati FM katika Kijiji cha Binguni Wilaya ya Kati Mkoa wa Kusini Unguja na Mradi wa Kimataifa wa Maendeleo ya Habari kupinga Ukatili Dhidi ya Wanawake na Wasichana (IPDC) wa UNESCO katika kijiji hicho.