The House of Favourite Newspapers

MAKAMU WA RAIS BENKI YA AFRIKA “DOLA 300M ZINAKUJA TANZANIA”

Rais John Pombe Magufuli, leo Ijumaa, Novemba 16, 2018 amekutana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia (Afrika), Dr. Hafez Ghanem, Ikulu jijini Dar es Salaam, ambaye ametangaza kuwa Benki ya Dunia imeridhia kutoa Dola za Marekani milioni 300 kwa ajili ya mradi wa kuongeza ubora wa elimu ya Sekondari.

“Hata zile Dola milioni 300 ambazo watu wasiotutakia mema walisema zimefyekelewa mbali hakuna lolote, Yeye (Makamu wa Rais Benki ya Dunia Afrika) amesema zipo na tutapewa” amesema Rais Magufuli.

Rais Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia kwa Kanda ya Afrika Hafez Ghanem mara baada ya kuwasili Ikulu jijini Dar es Salaam.

 

 

BENKI YA DUNIA imeridhia kutoa dola milioni 300 kwa Tanzania

Comments are closed.