The House of Favourite Newspapers

Makamu wa Rais Dkt. Mpango Afungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza Dodoma

0

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Mpango ameipongeza Wizara ya Mambo ya Ndani na Jeshi la Magereza kwa kuanza kuyafanyia kazi mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai ambapo amewahimiza kuyapokea na kuongeza kasi ya utekelezaji wake.

Makamu wa Rais Dkt. Mpango ameyasema hayo leo Oktoba 24, 2024 wakati akifungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza uliofanyika leo Oktoba 24, 2024 Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Msalato, Dodoma.

Dkt, Mpango amesema pamoja na mabadiliko ya Sheria yanayohitijika pia amewataka viongozi na maafisa wa magereza kubadili mtazamo ili kuendana mazingira ya sasa kwa kuwa mfumo na Sheria za magereza zimerithiwa kutoka kwa wakoloni, ambapo ameitaka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kuharakisha mchakato wa marekebisho ya Sheria kwa kuzingatia mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai na hali ya sasa. “matarajio ya Amiri Jeshi Mkuu na sisi Wasaidizi wake ni kuwa Mkutano huu usaidie kuleta mitazamo chanya ndani ya Jeshi la Magereza kuhusu mabadiliko”

Kwa upande wake Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Msauni, amesema Wizara itaendelea kusimamia marekebisho na maboresho ya Jeshi la Magereza ikiwa ni pamoja na kutenganisha majukumu ya urekebu ya Jeshi la hilo na majukumu ya kibiashara kufanywa na shirika la uzalishaji mali (SHIMA) “Maboresho ya Shirika hili la (SHIMA) litaisaidia Jeshi la Magereza kutumia rasilimali zilizopo ikiwemo ardhi ili iweze kuzalisha kwa tija na kwa ufanisi na Jeshi la hilo na kutatua changamoto zake mbalimbali na kujitosheleza kwa chakula na hata kutoa mchango kwa taifa”

Naye Kamishna Generali wa Jeshi la Magereza, CGP. Jeremiah Katungu amesema Jeshi hilo limeongeza uzalishaji wa mazao makuu kwa ajili ya wafungwa na mahabusu kutoka tani 1031 za mahindi, tani 340 za mpunga, tani 29 za maharage na tani 32 za mafuta ya alizeti kwa mwaka 2022/2023 hadi kufikia tani 1538 za mahindi, tani 737 za mpunga, tani 110 za maharage na tani 49 za mafuta ya alizeti kwa mwaka 2023/2024.

Leave A Reply