Makamu Wa Rais Dkt. Mpango Atembelea Hospitali Ya Benjamin Mkapa

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango, akimpa pole na kumfariji Bibi Leah Mahibwa (50) Mkazi wa Manyoni aliyelazwa kwa Matibabu katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma, wakati Makamu wa Rais alipofika katika Hospitali hiyo leo Mei 04,2021.

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango leo Mei 04,2021 ametembelea Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, akisalimiana na kuwapa pole Wananchi mbalimbali waliofika katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma kwa ajili ya kupatiwa Matibabu wakati Makamu wa Rais alipofika katika Hospitali hiyo leo Mei 04,2021.

Makamu wa Rais, Dkt. Philip Isdor Mpango, akipata maelezo kutoka kwa Daktari wa mambo ya Neuron Surgery Dr. Humba, kuhusu maendeleo ya Matibabu ya Bibi Zaveria Chuga Malamba (62) Mkazi wa Dodoma aliyelazwa kwa Matibabu katika Hospitali ya Benjamin Mkapa Jijini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akisindikizwa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango, alipokuwa akiondoka katika Uwanja wa Ndege Jijini Dodoma leo Mei 04,2021 kuelekea Nchini Kenya kwea Ziara ya Siku mbili.

(Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)Tecno


Toa comment