Makamu wa Rais Dkt. Nchimbi Afungua Semina Elekezi kwa Mawaziri na Manaibu Mawaziri Dar

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi amefungua Semina Elekezi kwa Mawaziri na Naibu Mawaziri inayofanyika katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere Jijini Dar es Salaam. Desemba 01, 2025.
Waziri Mkuu Dkt. Mwigulu Nchemba alishiriki katika ufunguzi huo.
Kauli mbiu ya Semina hiyo ni “Nafasi na Wajibu wa Mawaziri katika Utumishi wa Umma na kufikiwa kwa Malengo ya Dira ya Taifa 2050 na Ilani ya Uchaguzi 2025”.


