The House of Favourite Newspapers

Makamu Wa Rais Kuongoza Upandaji Miti Kesho dar

makonda-2Mkuu wa Mkoa wa Dar es Saalam Paul Makonda.

MAKAMU wa Rais, Samia Hassan Suluhu anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika
uzinduzi wa Kampeni ya Upandaji Miti Mkoa wa Dar es Salaam.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar leo, mkuu wa mkoa huo, Paul Makonda amesema kila mwananchi wa Dar anapaswa kupanda mti mmoja kwa ajili ya ustawi wa afya na mazingira.

Amesema zoezi hilo litazinduliwa rasmi na Samia Suluhu katika Barabara ya Kilwa kwenye Wilaya ya Temeke na baadaye watakagua miundombinu
ya maji kwa ajili ya umwagiliaji wa miti hiyo.

Makonda amesema miti hiyo itakayopandwa ni faida ya Mkoa wa Dar kwa ajili ya hewa pamoja na vivuli vya kupumzika hivyo amewataka wananchi kupanda miti yao katika maeneo yanayowazunguka pamoja na
watendaji wote wa mitaa na kata wa mkoa wa Dar.

Na Denis Mtima/GPL.

Comments are closed.