Makamu wa Rais Philip Mpango Awajibu Waliomzushia Kifo “Nawaombea Msamaha Kwa Mungu Awasamehe”- Video

Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk Philip Mpango amewashukuru Watanzania kwa kumuombea huku akibainisha kuwa alikuwa nje ya nchi kwa shughuli maalumu takribani mwezi mmoja.
“Asanteni sana kwa kuniombea, yamesemwa mengi si ndio? Na wengine bado wanasema mimi ni mzuka..

“Muwe na amani nipo salama nilikwenda nje kufanya shughuli malum takribani mwezi mmoja sijapungua hata kidogo si ndio?… Wapo wengi walioumizwa na maneno ambayo hayana msingi, wale waliokuwa wanatuma picha yangu na mshumaa pembeni…. wengine walisema mzee amekata moto…muda wangu bado,”amesema Dk Mpango.
Dk Mpango ameungana na waumini wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mwenyeheri Maria Theresa Ledochowska Kiwanja cha Ndege mkoani Dodoma katika Ibada ya Jumapili leo Desemba 10, 2023. Ibada hiyo imeongozwa na Padre Dionis Paskal Safari.
