The House of Favourite Newspapers

MAKAMU WA RAIS MAMA SAMIA SULUHU ATEMBELEA BANDA LA ZANTEL SABASABA

0
Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Mama Samia Hassan Suluhu (wa pili kulia) akipata maelezo kutoka kwa Mfanyakazi wa Kampuni ya Zantel alipotembelea banda la Kampuni hiyo katika maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba yanayoendelea hivi sasa katika viwanja vya Mwl J.K Nyerere. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na uwekezaji Mhe. Charles Mwijage na wa pili kushoto ni Meneja wa Data na Vifaa vya intaneti wa Zantel, Hamza Zuheri.
Meneja wa Data na Vifaa vya intaneti wa Zantel, Hamza Zuheri (wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Mama Samia Hassan Suluhu alipotembelea banda la Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel katika maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba yanayoendelea hivi sasa katika viwanja vya Mwl J.K Nyerere.
Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu akiangalia uchangiaji damu katika banda la Zantel katika maonesho ya biashara ya 41 ya biashara ya Kimataifa katika viwanja vya sabasaba jijini Dar es Salaam.Picha zote na Team Michuzi Sabasaba.
Meneja wa Data na Vifaa vya intaneti wa Zantel, Hamza Zuheri (wa pili kushoto) akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Mama Samia Hassan Suluhu alipotembelea banda la Kampuni ya Mawasiliano ya Zantel katika maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba yanayoendelea hivi sasa katika viwanja vya Mwl J.K Nyerere. Kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na uwekezaji Mhe. Charles Mwijage na wa pili kushoto ni Meneja wa Data na Vifaa vya intaneti wa Zantel, Hamza Zuheri.
Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Mama Samia Hassan Suluhu akimpongeza Mratibu wa Masoko wa Zantel-Zanzibar, Haji Khatib kwa kuchangia damu kwa hiari baada ya kiongozi huyo kutembelea banda la kampuni hiyo jana jijini Dar es salaam ili kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa. Zantel kwa kushirikiana na Mpango wa Taifa wa damu Salama wameandaa utaratibu wa uchangiaji damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu wenye uhitaji wa huduma hiyo katika kipindi hiki cha maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba yanayoendelea katika viwanja vya Mwl J.K Nyerere.
Makamu wa Rais wa Tanzania Mhe. Mama Samia Hassan Suluhu akisalimiana na Meneja wa Chapa na Mawasiliano wa Zantel, Rukia Mtingwa alipotembelea banda la Kampuni hiyo katika maonyesho ya 41 ya Kimataifa ya Dar es salaam maarufu kama Sabasaba yanayoendelea hivi sasa katika viwanja vya Mwl J.K Nyerere.
Leave A Reply