The House of Favourite Newspapers

SAMIA SULUHU AIPONGEZA BENKI YA NMB KWA MSAADA WA VIFAA VYA AFYA VITUO VYA AFYA KISARAWE VYENYE THAMANI MIL 15

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akipokea msaada wa vifaa vya hospitali kutoka kwa Mkuu wa kitengo cha Biashara za Serikali cha NMB, Vicky Bishubo kwa ajili ya vituo vya afya vya Maneromango, Chole na Kirui vya wilayani Kisarawe. Wa pili kutoka (kulia) ni Mkuu wa Wilaya ya Kisarawe, Jokate Mwegelo na wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano NMB, Joseline Kamuhanda.
…Samia Hassan Suluhu akiangalia mashine ya Oxygen iliyokabidhiwa na Benki ya NMB kwa kituo cha afya Maneromango wilayani Kisarawe mkoani Pwani.
Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan akiangalia moja ya kitanda cha kujifungulia kilichokabidhiwa na Benki ya NMB kwa kituo cha afya cha Maneromango wilayani Kisarawe mkoani Pwani.

 

 

MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ameishukru Benki ya NMB kwa kwa kutoa msaada wake wa mashuka 108, mashine za kupumulia wagonjwa, vitanda vya kujifungulia, na vitanda vya wagonjwa vyote vikiwa na thamani ya Shilingi Milioni 15 kwenye kituo cha afya cha Maneromango wilayani Kisarawe mkoani Pwani.

 

 

Akipokea vifaa hivyo aliushukuru ongozi mzima wa Benki ya Nmb kwa kuendelea kusaidia jamii katika suala zima la afya katika wilaya ya Kisarawe na maeneo mengine hapa nchini.

 

 

Mkuu wa kitengo cha Biashara za Serikali cha NMB, Vicky Bishubo alimkabidhi Makamu wa rais Samia Sluhu msaada  huo wa vifaa kwa ajili ya vituo vya afya vya Maneromango, Chole na Kirui vya wilayani Kisarawe.

 

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan alipokea msada hou mara baada ya ziara yake ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa barabara za lami Kisarawe mjini, ikiwa sehemu ya ziara yake ya siku sita ya kukagua na kuhamasisha shughuli za kimaendeleo mkoani Pwani.

 

 

Comments are closed.