The House of Favourite Newspapers

Makamu wa Rais wa Malawi afariki dunia katika ajali ya ndege

0

Taarifa kutoka Ofisi ya Rais ya Malawi imesema kuwa ndege iliyokuwa imembeba Makamu wa Rais wa nchi hiyo, Saulos Chilima na watu wengine tisa imetoweka baada ya kuondoka katika mji mkuu Lilongwe, Juni 10, 2024.

Rais Lazarus Chakwera amearifiwa kuhusu tukio hilo na kuamua kufuta ziara yake nchini Bahamas na kuamuru vyombo vyote nchini humo kushiriki katika kuitafuta ndege na kufanya uokoaji.

Tayari juhudi za kuitafuta ndege zimeanza lakini bado haijapatikana tangu kukatika kwa mawasiliano saa nne asubuhi za Malawi.

Leave A Reply