The House of Favourite Newspapers

Makanisa Matatu Yachomwa Moto Bukoba

0

1

Kanisa lilivyoteketea kwa moto.
3
Kinanda kinchotumiwa na wanakwaya kwa ajili ya kupigia muziki kikiwa kimeungua.4 5Makanisa hayo baada ya kuteketezwa kwa moto. 6Waumini wa makanisa hayo wakiwa wamekusanyika kushuhudia tukio hilo. 7

Mabaki ya kanisa baada ya kuteketezwa kwa moto.8Mmoja wa viongozi wa makanisa hayo akizungumza wa waandishi wa habari baada ya kukuta kanisa lake limechomwa moto.

WATU wasiojulikana wamechoma makanisa mtatu mjini Bukoba leo. Makanisa yaliyochomwa moto ni Pentecostal Assemblies of God (PAG) eneo la Buyekera, Living Water International na Evangelical Assemblies of God (EAGT) kata ya Kibeta yote ya mjini Bukoba.

Wachungaji na viongozi wa kiroho wa makanisa hayo wametoa wito kwa vyombo vya dola kuwabaini wahusika wa tukio hilo linaloashiria  uvunjifu wa amani.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Augstine Oromi, amethbitisha kutokea kwa tukio hilo  na kusema kuwa atatoa tamko rasmi baadaye.

Matukio ya makanisa kuchomwa yameshamiri katika Manispaa ya Bukoba, ambapo hili ni tukio la sita la kuchoma moto nyumba za ibada kwa kipindi cha mwaka mmoja.

NA JAMII FORUM

JIUNGE NA GLOBAL BRAKING NEWS UPATE HABARI KEMKEM ZA UCHAGUZI MKUU

globalbreakingnews.JPG

Leave A Reply