Makazi Ya Wema Mbagala Yashtua!

SUPASTAA wa Bongo Movies, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’ hivi karibuni amezua taharuki baada ya makazi yake yaliyopo Mbagala-Kijichi jijini Dar, kushtua watu wengi, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA linaripoti.

 

MJENGO WA KAWAIDA…

Mjengo huo ambao unaonekana ni wa kawaida mno, tofauti na alivyozoeleka kuishi kwenye mijengo ya kifahari ushuani, safari hii mambo ni tofauti.

 

Wengi wanadai kwamba, mjengo anaoishi Wema kwa sasa hauna hadhi yake hivyo kumshangaza kila mtu hasa mashabiki wake ambapo kila mmoja anahoji nini kimemkuta hadi kufikia hali hiyo?“

 

Jamani juzi tu Wema alikuwa anaishi Masaki (Dar), tena kwenye bonge la mjengo, lakini leo hii eti anaishi Kijichi (Mbagala), tena kwenye nyumba ambayo haina hadhi ya kistaa kama alivyozoeleka, sisi huwa tunamuona hapa hafananii kwa kweli, kama hamuamini njooni mjionee wenyewe,” alisema sosi mmoja kwa sharti la kutotajwa gazetini.

 

SOSI MWINGINE…

“Huyu dada amefulia vibaya mno jamani, hii nyumba anayoishi hapa, hapana kwa kweli, haendani nayo hata kidogo, kweli maisha ni kama mlima kupanda na kushuka na yanabadilika haraka mno,” mdau mwingine aliongeza.

OFM KAZINIIli kupata ukweli wa mambo yote hayo, Gazeti la IJUMAA WIKIENDA lilituma kikosi-kazi chake cha OFM (Operesheni Fichua Maovu) ambacho kilifunga safari hadi nyumbani kwa mrembo huyo huko Kijichi jijini Dar na kujionea mambo kibao yasiyofanana na hadhi ya jina la Wema ambaye anashikilia taji la Miss Tanzania mwaka 2006/07.

 

MAJIRANI WAZUNGUMZA…

Kabla ya kuingia ndani ya nyumba hiyo kwa kutoamini kama kweli Wema anaishi mahali hapo, mashushushu wetu waliongea na baadhi ya majirani ambao walithibitisha mrembo huyo kuishi kwenye nyumba hiyo.“Ni kweli Wema anaishi hapa tangu mwaka jana mwezi wa nane, tena haishi peke yake, anaishi na vijana wengi tu, hata bethidei yake ya mwaka jana alisherehekea hapahapa na tukala keki.

 

“Ni mtu poa sana, hana makuu, akipita na gari lake anashusha kioo na kusalimia majirani, ila sisi wenyewe tunashangaa kwa nini amekuja kuishi kwenye nyumba kama hii kwa sababu haiendani na yeye hata kidogo kutokana na ukubwa wa jina lake,” alisema jirani mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Sabrina na kuongeza;“Lakini tunafurahi kuishi na Tanzania Sweetheart (Wema).

”IJUMAA WIKIENDA LABISHA HODI

Baada ya kumaliza kuzungumza na baadhi ya majirani, waandishi wetu walibisha hodi getini kwa muda mrefu bila kufunguliwa.

 

Makachero wetu kwa kutumia kamera zenye uwezo mkubwa walifanikiwa ‘kuzoom’ mazingira ya ndani kupitia kwenye upenyo wa geti.Kamera zilinasa mazingira ambayo si mazuri kivile ndani ya geti huku vitu vikiwa vimekaa bila mpangilio kuonesha ni nyumbani kwa staa mkubwa Bongo.

Baada ya kupiga picha kadhaa, waandishi wetu walipiga hodi kwa mara nyingine na safari hii walifunguliwa na kuingia ndani ambapo walikuta vijana wengi wa kike kwa wa kiume wakifanya shughuli mbalimbali ambapo mambo yalikuwa hivi;

IJUMAA WIKIENDA: Hodi…

MWANADADA: Karibuni…

 

IJUMAA: Asante, samahani hivi hapa ndipo anapoishi Wema?

 

MWANADADA: Ndiyo, ndipo hapa…

 

IJUMAA WIKIENDA: Ahaa! Vipi tumemkuta?

MWANADADA: Hapana, ametoka, tena mmepishana naye muda si mrefu, ameenda mjini.

 

IJUMAA WIKIENDA: Okey, basi sawa tutarudi wakati mwingine.

MWANADADA: Sawa, ila ninyi ni akina nani?

 

IJUMAA WIKIENDA: Ooh! Sisi ni waandishi wa habari, tunatoka Gazeti la IJUMAA WIKIENDA, tulitaka kufanya naye mahojiano kidogo…

MWANADADA: (anakunja sura) Poa…Baada ya hapo kunakuwa na sintofahamu ya wahusika kuitana na kuonekana kuulizana ni nani aliyewaelekeza waandishi wetu kufika mahali hapo.

 

MAKACHERO WASEPA

Hata hivyo, waandishi wetu waliaga na kuondoka huku wakiwaacha watu hao wakishangaa bila kujua mshangao wao ulitokana na nini?

 

TUJIKUMBUSHE

Wema ameshakaa kwenye mijengo mbalimbali yenye hadhi kwa miaka ya nyuma ikiwemo ile ya Kijitonyama, Salasala, Ununio na Masaki ambayo alikuwa akilipa mamilioni ya kutosha kwa mwaka tofauti na nyumba ambayo anakaa kwa sasa.Nyumba hiyo anayokaa kwa sasa, inakadiriwa kuwa na kodi isiyozidi shilingi laki nne kwa mwezi wakati zile za awali, zilikuwa zinacheza kwenye shilingi milioni moja na zaidi kwa mwezi.

⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx

Toa comment