The House of Favourite Newspapers

Makonda Ampa Maagizo Mkandarasi wa Mwendokasi ya Mbagala

0

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam,  Paul Makonda, amemtaka mkandarasi wa mradi wa ujenzi wa Barabara ya Mabasi ya Mwendokasi kutoka katikati ya jiji kuelekea Mbagala, kuongeza kasi ili mradi huo wenye kugharimu zaidi ya Sh. bilioni 200 ukamilike na kupunguza kero ya usafiri kwa wananchi wa eneo hilo.

 

Makonda ameyasema hayo leo alipokuwa anakagua maendeleo ya mradi huo ambapo alielezea kuwa wakazi wa Mbagala wamekuwa wakipata changamoto ya usafiri ka muda mrefu zikiwemo foleni na wakati mwingine  kuibiwa vitu mbalimbali wakati wa kugombania usafiri.

 

Kukamilika kwa barabara hiyo kutafanya Barabara ya Kilwa kuwa na njia sita, madaraja mawili makubwa na njia ya juu (flyover),  jambo litakalosaidia kurahisisha shughuli za usafiri.

 

Amezungumaia pia changamoto ya mafuriko Mto Msimbazi kujaa eneo la Jangwani na kusababisha kusimama kwa shughuli za usafiri ambapo amesema serikali ipo katika hatua ya kuanza kwa maboresho ya eneo hilo ikiwa ni pamoja na kuinua daraja lililopo na kuufanya Mto Msimbazi kuwa sehemu ya utalii wa boti ambapo ujenzi unatarajiwa kugharimu kiasi cha Sh.  bilioni 200.

 

Kuhusu ugonjwa wa Corona,  amesema tayari amewaelekeza wakuu wa wilaya kuhakikisha wanatenga maeneo maalum ya kuwahifadhi watu wote wanaotoka nje ya nchi (karantini) ili wakae chini ya uangalizi kwa muda wa siku 14 huku akiwahimiza wananchi kuendelea kuchukua tahadhari dhidi ya maambukizi ya virusi hivyo vya Corona.

Leave A Reply