MAKONDA AMUOMBEA RUGE JUKWAANI FIESTA (PICHA +VIDEO)

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akiwa katika Tamasha la Fiesta usiku wa kuamkia leo katika Viwanja vya Posta, Kijitonyama, Dar.

…Akisikiliza historia ya Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji Clouds FM, Ruge Mutahaba.

…Akiendesha maombi ya kumuombea Ruge.

Umati uliohudhuria tamasha ukiendesha maombi.

Makonda akiongea jambo

 

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, usiku wa kuamkia leo ameshuhudia Tamasha la Fiesta katika Viwanja vya Posta, Kijitonyama Dar es Salaam.

Makonda alitumia fursa hiyo kusikiliza historia Mkurugenzi wa Vipindi na Uzalishaji kituo cha Clouds FM, Ruge Mutahaba,  pamoja na kumuombea apone haraka na kurejea kwenye majukumu yake kwa kuwa ana mchango mkubwa wa kuibua fursa mbalimbali kwa vijana.

Ruge ni mgonjwa ambaye anaendelea na matibabu nchini Afrika Kusini.

Pia ametumia muda huo kumpongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri anayoifanya kwa Watanzania kwa miradi na mikakati mbalimbali ya kupanua barabara katika Jiji la Dar es Salaam

(PICHA: RICHARD BUKOS, GPL)

Loading...

Toa comment