The House of Favourite Newspapers

MAKONDA AMWAGA MACHOZI MBELE YA FAMILIA ILIYOTAPELIWA NYUMBA  

Mkuu wa  Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda (kushoto) akiambatana na wanafamilia inayodaiwa kutapeliwa nyumba yao baada ya kuwatembelea  eneo wanaloishi kwa sasa huko  Kunduchi.

Mkuu wa Mkoa wa Dares Salaam, Paul Makonda amemwaga machozi alipoitembelea familia ya Stela Bujumula baada ya kuelezwa jinsi inayoishi kwa kutangatanga, kufuatia kutapeliwa nyumba yao iliyopo Kunduchi jijini Dar es Salaam, na kuahidi kutoa msaada wa kisheria ili warejeshewe nyumba yao.

 

 

Mkutano na wanahabari ukifanyika.

Baada ya wanafamilia hiyo kumueleza jinsi walivyotolewa kwenye nyumba yao kwa madai ya kushindwa kulipa deni la mkopo waliochukua katika Benki ya CRDB na nyumba hiyo kupigwa mnada, Makonda ambaye ametoa msaada wa vyakula kwa familia hiyo kwa ajili ya kujikimu, amesema atahakikisha sheria inachukua mkondo wake.

 

 

Mama wa familia hiyo aitwaye, Stela Bujumula akimweleza Makonda juu ya sakata hilo.

Akizungumza mbele ya mkuu wa mkoa, mmiliki wa nyumba hiyo, Stela Bujumula alisema kwa takribani miaka sita sasa, familia yake inateseka baada ya nyumba hiyo kupigwa mnada, katika mazingira ya liyojaa utata.

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akizungumza na waandishi wa habari  kuhusiana na maelezo aliyopokea kutoka kwa familia hiyo.

 

Ameitaka familia hiyo kufika ofisini kwake, Ilala jijini Dar es Salaam, Jumatatu ya Januari 29, wakiwa na nyaraka zote muhimu kwa ajili ya kuanza kulifuatilia sakata hilo kuhakikisha haki inatendeka.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikabidhi zawadi ya vyakula kwa familia inayodaiwa kutapeliwa nyumba.

 

Nyumba inayodaiwa kuwa ya familia iliyotapeliwa kama inavyoonekana.

 

Baadhi ya vyakula alivyoipata familia hiyo.

…Akitoa machozi mbele ya familia hiyo.

NA DENIS MTIMA | GLOBAL PUBLISHERS

Makonda Amwaga Machozi Mbele Ya Familia Iliyotapeliwa

Comments are closed.