MAKONDA AMWAMBIA JPM – “Nikiwa Mkubwa Nataka Kuwa Wewe” – Video

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewaomba viongozi wa dini wamuombee ili atimize ndoto ya kuwa kama Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli.

 

Makonda amesema hayo leo Ijumaa, Januari 11, 2018 katika mapokezi ya ndege mpya ya Air Tanzania aina ya Airbus A220-300 kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar, Makonda amewataka viongozi wa dini kumuombea juu ya ndoto yake ya kuwa kama Rais Magufuli kwa kuwa ni mtu wa kutekeleza na haogopi kufanya maamuzi.

 

“Viongozi wa dini naomba mniombee, nataka nikikua niwe kama Rais Magufuli, haya ni maombi yangu kabisa, kwa sababu ni mtu wa kutekeleza, usiyeyumbishwa,umehakiksha Mungu kwanza na unaipenda Tanzania kuliko hata familia yako.

 

“Hivi ulivyo Rais wetu angekuwa mwingine Watoto wake tungekuwa tunagombana nao mtaani lakini Wewe umehakikisha hakuna anayeingilia jukumu lako kama Baba wa familia,” amesema Makonda.

 

Pamoja na hayo Makonda amemwambia Rais Magufuli, yeye na wakazi wa Dar es salaam wamekwenda kumuunga mkono kwa kuwa alitoa ahadi kutoka kwenye ilani ya CCM na anatekeleza ikiwemo elimu bure.

VIDEO: MSIKIE MAKONDA HAPA AKIFUNGUKA

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Loading...

Toa comment