The House of Favourite Newspapers

Makonda Angekuja Mapema… Wakali Hawa Wasingepotea

Geneza la Marehemu Langa Kileo

GUMZO kubwa kunako burudani nchini ni juu ya mastaa wa Bongo kutuhumiwa kuhusika na matumizi ya madawa ya kulevya. Wikiendi iliyopita upepo ulivuma vibaya kwa baadhi yao baada ya kuitwa na kuhojiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kwenye Kituo Kikuu cha Polisi jijini Dar.

Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akiwa ofini kwake
Wema Sepetu katika pozi

Makonda aliyeteuli­wa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Machi 13, mwaka jana aliwataja wanaotuhu­miwa kutumia madawa ya kulevya wakiwemo TID, Wema Sepetu, Chid Benz, Nyandu Toz , Recho na wengineo huku akiwataka kufika Ijumaa (wiki iliyopita) katika Kituo Kikuu cha Polisi, jambo lililotekelezwa na baadhi yao.

Kwanza Wikienda linam­pongeza Makonda aliyewahi pia kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, kwa uamuzi wake wa kujitokeza hadharani na kuwataja baadhi ya askari wa jeshi la polisi pamoja na wasanii maarufu hapa nchini wanaotuhumiwa kuhusika na mtandao wa biashara hiyo haramu ya madawa ya kulevya.

Biashara hii haramu ya mad­awa ya kulevya ni janga kubwa la kidunia kwa muda mrefu ambapo kundi la wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya na vijana wa kimas­kini wamekuwa ni waathirika wakubwa, hali inayotishia nguvu kazi ya Taifa.

Wapo wasanii wengi wakubwa duniani kama Elvis Presley na Whitney Houston waliopoteza uhai kwa matumizi ya madawa hayo lakini pia ukiachana na wasanii hao, nchini Tanzania pia katika tasnia ya Bongo Fleva, wapo wasanii am­bao wameathirika na kukimbizwa kwenye vituo maalum vya kuhudumia waathirika wa madawa hayo (sober hosues) na wengine kutangulia mbele za haki wakiwa bado na umri mdogo mno.

Katika makala haya, nimekucha­mbulia baadhi tu ya wasanii hao ambapo kama Makonda angekuja mapema (miaka 10 iliyopita) wakali wengi wa muziki wasingepotea;

Rashid Makwilo ‘Chiddy Benz’

CHID BENZ

Ni mmoja kati ya wakali wa Hip Hop Bongo kuwahi kutokea. Chid aliyewahi kubamba na ngoma nyingi kali kama Dar Stand Up (Ngoma Itambae), Nihurumie na Mashaalah anaingia katika listi ya waathirika wa madawa haya ilihali mashabiki wake wakiwa wana­tamani kuendelea kusikia midundo na floo zake.

Mwaka jana, Chid aliweka wazi kusaidiwa kutokana na kupungua mwili kutokana na matumizi hayo ambapo alipele­kwa sober house Bagamoyo mkoani Pwani. Hata hivyo, baada ya kutibiwa kwa siku 28 alitoka lakini baada ya siku kad­haa akarudia tena kubwia madawa hayo hali iliyomfanya kuendelea kuwa muathirika.

Nando

NANDO

Mshiriki huyu wa Shindano la Big Brother Africa 2014 ‘The Chase’ ame­ingia kwenye listi ya mastaa walioji­ingiza katika matumizi ya dawa hizo kisha kumtoa kwenye reli ya ndoto kubwa ya kufanikiwa kimaisha.

Nando anayetambulika pia kwa jina la Ammy, aliwahi kutangaza kutumia madawa ya kulevya kwa muda mrefu kisha kuamua kuacha lakini hivi karibuni picha mbalimbali zilizagaa mitandaoni zikimuonesha hali yake ilivyokuwa baada ya kuathirika na matumizi ya dawa hizo.

Kwa sasa yupo chini ya kituo cha kutibu waathirika wa madawa ya kulevya (jina linahifadhiwa).

Marehemu Langa Enzi za Uhai wake

LANGA

Langa Kileo ambaye ni chimbuko la Coca-Cola Pop Star mwaka 2004, alifariki dunia Juni, 2013 kwa kile kilichoelezwa ni malaria.

Maisha ya Langa kimuziki yalianza kuporomoka pale alipoachia albamu yake ya ‘Langa’ na kushindwa kuuza baada ya kukataliwa na wasam­bazaji na kuamua kujiingiza kwenye maisha ya uteja ya utumiaji wa madawa ya kelevya.

Baada ya jitihada za familia yake alifanikiwa kuchomoka kwenye ma­tumizi ya madawa hayo na kuachia ngoma kama Mteja Aliyepata Nafuu ambapo kwa sasa mwili wake ume­lala kwenye Makaburi ya Kinondoni jijini Dar.

Marehemu Albert Mangwea enzi za uhai wake

NGWEA

Mmoja kati ya wakali wa Bongo Fleva kuwahi kutokea aliyekuwa akitamba mwanzoni mwa miaka ya 2000 na ngoma kibao kama vile Mikasi, Ghetto Langu, Spidi 120 na nyingine kibao zilizokuwa nyimbo za taifa.

Ngwea alikuwa akituhumiwa kutumia madawa ya kulevya kwa muda mrefu kabla ya kukutwa na umauti Mei, 2013 katika Hospitali ya St. Hellen huko Johannesburg, Afrika Kusini.

Kwa mujibu wa ripoti baada ya kufikishwa hospitali, sampuli zilizo­patikana mwilini mwake zilionesha mkusanyiko wa madawa ya kulevya kama heroine, cocaine chafu na bangi ambavyo vilikutwa kwenye damu yake ambapo kwa sasa mwili wake umepumzishwa kwenye Maka­buri ya Kihonda mjini Morogoro.

Wapo wasanii wengi ambao walitu­mia, kutuhumiwa kutumia madawa ya kulevya na wengine kukutwa na umauti kama Banza Stone, Aisha Madinda, Geez Mabovu na wengi­neo.

Wengine wanaotuhumiwa kupotea kwenye ubora wao kisa madawa ya kulevya ni pamoja na Dogo Mfaume, Rachel wa THT, Msafiri Diouf, Lord Eyez, Ray C, Young D na wengine kibao ambao kama angetokea kion­gozi aliyeanzisha vita hiyo mapema kwa vitendo wangesalimika.

Comments are closed.