The House of Favourite Newspapers

Ni Majonzi, Simanzi Vyatawala Kuagwa kwa Joel Bendera (Pichaz + Video)

Mwili wa Bendera ukipelekwa eneo maalum kwa ajili ya kuagwa.

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewaongoza mamia ya watu waliojitokeza  kumuaga aliyewahi kuwa kocha wa Taifa Stars, Joel Bendera katika Viwanja  vya Hospitali ya Lugalo jijini Dar  ambaye anatarajiwa kuzikwa kesho Korogwe, Tanga.

 

Waombolezaji wakiwa wenyehudhuni.

Bendera  aliyefariki Jumatano wiki hii  katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili aliwahi kushika nyadhifa tofauti serikali ikiwemo ili ya Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mbunge wa  Korogwe  Mashariki na Mjini na  baadaye kuwa Mkuu wa mkoa wa Morogoro na Manyara.

Mwili ukiingizwa kwenye gari tayari kwa safari ya Tanga kuzikwa.

Simanzi na majonzi vimetawala wakati wa kuaga mwili wa kiongozi huyo ambaye pia alikuwa mchezaji wa zamani wa Timu ya Taifa na Kocha Mstaafu.

Viongozi wa TFF wa sasa na wastaafu wakijadiliana jambo wakatiwa kuaga mwili huo.

 

Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akiwa na waombolezaji wengine.

 

Mkuu wa Mkoa Paul Makonda akipita kuaga mwili wa marehemu Bendera.

 

Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiaga mwili wa marehemu.

 

Katibu Mkuu wa Yanga, Charles Boniface Mkwasa akiaga mwili.

 

Msemaji wa TFF, Alfred Lucas akiaga.

 

Mbunge wa Sengerema na Waziri wa zamani wa Nishati na Madini, William Ngereja akitoa pole kwa waombolezaji.

 

Ndugu wa marehemu wakiaga.

 

MUSA MATEJA/GPL.

 

VIDEO YA KUAGA MWILI WA BENDERA

Comments are closed.