The House of Favourite Newspapers

Makonda aongoza upimaji magonjwa ya moyo Dar

0

17

Makonda akihojiwa na wanahabari leo wakati wa zoezi la upimaji wa magonjwa ya moyo uliofanyika bure na madaktari kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), katika viwanja vya Leaders Club Dar.

2

Mkuu wa Kitengo cha Moyo wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Dk. Peter Kisenge (kushoto) akizungumza na wananchi kabla ya zoezi la upimaji kuanza.

4

12

Umati wa wananchi waliojitokeza kupima afya zao.

6 7. 8 9 10

  Huduma zikianza kutolewa kutoka kwa madaktari hao.13

Hapa ni sehemu ya kupata msaada wa huduma mbalimbali.

14

Makonda (kulia) akishuhudia namna wagonjwa wanavyopatiwa majibu baada ya kumaliza kupatiwa matibabu.

15

Madaktari wakimsaidia mgonjwa aliyezidiwa ili kupelekwa Hospitali ya Muhimbili.

16

Mgonjwa huyo akiingizwa kwenye gari maalum kupelekwa Muhimbili.

MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Mkaonda, leo ameongoza wananchi wa wilaya yake na wakazi wengine wa jiji la Dar es Salaam katika upimaji wa magonjwa ya moyo uliofanyika bure na madaktari kutoka Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI), katika viwanja vya Leaders Club Dar.

Akizungumza na wanahabari, Makonda kwenye zoezi hilo amesema kuwa wananchi waliojitokeza wataweza kupata fursa ya kubaini magonjwa mbalimbali kwani wengi hawajui magonjwa ya moyo jinsi yanavyoweza kusababishwa na shinikizo la damu ikiwa ni chanzo cha magonjwa ya macho kiharusi, figo na hata kutokuzaa.
Amesema ugonjwa wa moyo ni hatari na asilimia kubwa ya wagonjwa hao wanatembea na kufanya kazi zao kwa kuwa ugonjwa huo hauna dalili ya haraka na hivyo ni vyema kila mmoja kupima na kujua afya yake.
Amesema wagonjwa watakaokutwa na magonjwa yanayoshabihiana na moyo watapatiwa tiba katika hospitali za jiji la Dar ikiwemo Hospitali ya Kinondoni ya Mwananyamala, na wale watakaokutwa wamethirika zaidi na ugonjwa huo watapelekwa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Aidha aliwataka wananchi kuelewa matibabu yake ni gharama kubwa hasa kwa wale wanaosafirishwa kupelekwa nje ya nchi. Zoezi hilo ni la siku moja lakini kutokana idadi ya wananchi waliojitokeza kuwa wengi zoezi hilo linaweza kuendelea hadi kesho mpaka idadi ya namba za wanaohitaji huduma zitakapomalizika.

HABARI/PICHA: DENIS MTIMA/GPL

Leave A Reply