The House of Favourite Newspapers

MAELFU WAFURIKA TAMASHA LA ‘KOMAA CONCERT 2018’ DAR


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  akihutubia maelfu ya wananchi waliofika kwenye tamasha la ‘Komaa Concert 2018’ lililotayarishwa na kituo cha radio cha Efm katika viwanja vya Tanganyika Packers, Dar es Salaam.
…Akichombeza neno.
Mwanamuziki wa Hip Pop nchini, Roma Mkatoliki,  akiimba na mashabiki.

Mr Blue,  akiimba.

Amber Lulu.
Nandy.

 

 

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda,  jana ameungana na maelfu ya wakazi wa jiji hilo kwenye tamasha kubwa la burudani lijulikanalo kama ‘Komaa Concert 2018’ lililoandaliwa na kituo cha utangazaji cha EFM/TV E ambapo amesema serikali ya mkoa wake itaendelea kutoa ushirikiano kwa wasanii kwa kuwa sanaa ni ajira rasmi inayowasaidia vijana wengi.

 

Akizungumza na maelfu ya wananchi,  Makonda amewaomba waendelee kumpa ushirikiano wa kutosha Rais John Magufuli huku akipongeza maendeleo makubwa yaliyopatikana tangu serikali ya awamu ya tano ilipoingia madarakani.

 

Aidha amewapongeza EFM kwa kuandaa tamasha hilo lililotoa fursa kwa wananchi wanyonge kupata burudani huku akiwakumbusha wananchi kuhakikisha wanafanya usafi wa mazingira kwenye maeneo yao wanayoishi.

Pia amewahimiza wananchi kuhakikisha wanalinda amani na usalama na kuwakumbuka kwenye maombi viongozi wote wa taifa.

Comments are closed.