Makonda Atembelea Walioathirika Na Mafuriko (Picha +Video)

Mkuu wa mkoa wa Dar es alaam, Paul Makonda leo ametembelea sehemu zilizoathiriwa na mvua kali iliyonyesha jana karibu mji mzima na kusababisha mafuriko baadhi ya sehemu. Katika ziara hiyo alianzia na Kigogo mwisho, Legho Sinza, Sweet Corner Manzese na kumalizia Jangwani.

Mkuu wa mkoa wa Dar es alaam, Paul Makonda leo ametembelea sehemu zilizoathiriwa na mvua kali iliyonyesha jana karibu mji mzima na kusababisha mafuriko baadhi ya sehemu. Katika ziara hiyo alianzia na Kigogo mwisho, Legho Sinza, Sweet Corner Manzese na kumalizia Jangwani.

Makabati haya yalikutwa pembezoni mwa mto eneo la Kigogo Mwisho yakiwa hayana mwenyewe.

Katika ziara hiyo alijionea uharibifu wa miundombinu kama vile barabara, madaraja, nguzo za umeme n.k. ambapo amewataka wakazi wa jiji kutojenga sehemu hatarishi.

 

Makonda pia aliwataka wakazi wa maeneo hayo kuacha kutupa takataka mtoni ambazo nyingi zimekuwa zikiziba madaraja na kusababisha maji kushindwa kupita kiurahisi na kurudi maeneo ya makazi.

Maduka eneo la Legho Sinza baada ya kuharibiwa na mafuriko na bidhaa zilizokuwemo kusombwa na maji.

Mkuu huyo wa mkoa pia aliwalaumu wanaochimba mchanga kwenye mito na kusema hao ndiyo chanzo cha mmomonyoko wa udongo na uharibifu wa mazingira.

Mmoja wa wakaanga chipsi akiwa ameokoa bidhaa zake.

Mafuriko pia yamesababisha kujaa tope katika barabara Morogoro eneo la Jangwani na hali iliyopelekea barabara hiyo kufungwa ili kupisha zoezi la kuondoa tope kwenye barabara hiyo.

 

Wanahabari wetu wakiwa eneo hilo walishuhudia greda likisafisha barabara hiyo kwa kuondoa tope lililojaa kwenye barabara hiyo.

Makonda akichanja mbuga eneo la Tandale Sweet corner kuelekea daraja la kutokea Shule ya Msingi ya Mama Salma Kikwete.

Wakazi hawa walinaswa wakivuka Mto Ng’ombe wakitoka eneo la Shule ya Msingi Salma Kikwete kwenda Tandale Sweet corner.

Makonda akizungumza na mama aliyeathiriwa na mafuriko.

Greda likizoa tope barabara ya Morogoro eneo la Jangwani ili njia hiyo iliyofungwa iweze kupitika.

HABARI: RICHARD BUKOS


Toa comment