Makonda Atibua 40 ya Mdogo wa Tiffah…

Diamond Platnumz

Na WAANDISHI WETU| AMANI| HABARI

DAR ES SALAAM: Ikiwa imebakia saa 72 ifike 40 ya mtoto wa pili wa Mbongo Fleva,  Nasibu Abdul ‘Diamond’, Nillan, shughuli hiyo imeingia mdudu baada  ya baadhi ya wanafamilia ya  mwanamuziki huyo kutangaza kutohudhuria sherehe hiyo kutokana na  wahusika wengine kukumbwa na msukosuko mkubwa wa kutajwa na kufikishwa kortini kwa madai ya kujihusisha na madawa ya kulevya (unga) kwenye oparesheni ya kutokomeza matumizi ya madawa hayo iliyoanzishwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.

SHEREHE IMEJITANGAZA

Sherehe hiyo ambayo imekuwa gumzo kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii, imepangwa kufanyika Jumamosi hii nyumbani kwa Diamond, Madale jijini hapa na inaaminiwa kuwa, wahudhuriaji watakuwa wengi wakiwemo mastaa wa Bongo.

MSIKIE HUYU

“Jamani Makonda ni balaa, hivi mnajua kuwa, kuna hatihati ya 40 ya Nillan kutofanyika au kufanyika bila mbwembwe nyingi? Iko hivi, mpaka sasa familia inasumbuka kuangalia namna ambavyo amani itarejea na mambo yawe kama kawaida.

“Unajua, oparesheni ya Makonda iliwagusa watu wawili wa familia hiyo. Ilimgusa shemeji wa Diamond, Petit Man (Ahmed Hashim) ambaye ni mume wa Esma lakini pia ikamgusa mdogo wa Diamond, Romeo George ‘Rommy Jones’. Rommy ni mtoto wa dada wa mama Diamond.

“Sasa kuwepo kwa wote wawili kwenye tukio moja, kumeifanya MAKONDA ATIBUA 40 familia hiyo kushindwa kushughulikia hata maandalizi ya 40 hiyo. Kwa hiyo kama nilivyosema, kama itafanyika lakini si katika ubora wake,” kilisema chanzo hicho.

MRATIBU WA SHUGHULI

Ikazidi kudaiwa kuwa, mratibu mkuu wa 40 ya Nillan ni Esma ambaye ni shangazi mtu lakini siku za maandalizi, ndiyo yakatokea ya kutokea.

ZARI ALISHATUA Habari za uhakika ni kwamba, mzazi mwenziye Diamond, Zarina Hassan ‘Zari’ tayari yupo jijini hapa tangu Jumapili iliyopita kwa ajili ya shughuli ya Nillan ambayo ilibuma kufanyika Afrika Kusini anakoishi Zari kwa sababu ambazo hazijawa wazi licha ya kuwepo kwa matangazo kibao.

Zarina Hassan Mama Millan

MAKAMPUNI YAMESHAJIPANGA

Makapuni matatu yameshajitokeza kudhamini 40 hiyo ambapo mtoto huyo kwa mara ya kwanza atafunuliwa uso na kuonekana na watu mbalimbali.

KAMA HAITAFANYIKA

Endapo shughuli hiyo haitafanyika kabisa, itakuwa ni pigo kwa Nillan baada ya kushindwa kufanyika kwa tarehe muafaka, Januari 16, mwaka huu.

AMANI LAMSAKA ESMA

Gazeti la Amani, juzi  lilipata nafasi ya kuzungumza na Esma ambaye muda wote alikuwa hana raha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akifuatilia ishu ya mumewe huyo ambapo alipoulizwa kuhusu 40 ya Nillan alisema kuwa, akili yake haifikirii kabisa kuhusu sherehe hiyo badala yake inawaza sakata la mumewe litaishia wapi hivyo hawezi kwenda kwenye sherehe hiyo.

“Mimi hapa ndugu yangu wala sifikirii kabisa kuhusu hiyo sherehe yaani na hili sekeseke la mume wangu sitoweza kwenda maana mwenzangu ndiyo katoka kwenye matatizo makubwa kiasi hicho hivyo nitaona picha tu kwakweli,” alisema Esma.

DIAMOND NA SIMU YAKE

Diamond alipopigiwa simu, hakupokea licha ya kurudiwa mara kwa mara kwa siku ya juzi.

MAMA DIAMOND NAYE Pia,

Amani lilipata nafasi ya kuzungumza na mama wa Diamond, Sanura Kasim ‘Sandra’ kuhusu ishu hiyo ambapo hali ilikuwa hivi. Mama Diamond: (Baada ya kupigiwa simu) enhe, niambie (anamtaja jina mwandishi). Kuna udaku gani huko kwako? Maana wewe ukinipigia lazima kuwe na udaku tu.

Nakusikiliza.

Amani: Kuna madai kwamba, shughuli ya mjukuu wetu inaweza isifanyike kutokana na wanafamilia kuwepo kwenye msukosuko wa oparesheni ya Makonda, ni kweli? Mama Dia

Mama Diamond: We nani amekwambia habari hizo?

Amani: Nimezisikia tu kutoka kwenye chanzo changu. Kweli si kweli?”

Mama Diamond: We kama unataka kuandika andika hivyohivyo ulivyosikia, mimi wala sina neno kabisa.

Amani: Sawa, sasa naomba kuongea na Diamond kama yupo.

Mama Diamond: Lazima namba zake unazo, mpigie mwenyewe.

Amani: Hapokei simu.

Mama Diamond: Mpigie tu au mtumie meseji.

Amani: Oke, basi msalimie mjukuu Nillan na mama yake, Zari si wapo hapo?”

Mama Diamond: Zimefika, wapo.

ZARI ASHTUKA

Habari zaidi zinasema kuwa, Zari baada ya kusikia Petit Man na Rommy ambaye pia ni DJ wa Diamond, wamedakwa na Makonda kwa unga, alishtuka sana na kutojua hatima yake.

WAMEFIKAJE HAPA?

Mbali na Petit Man na Rommy, wengine waliopandishwa kortini Kisutu juzi ni Khaleed Mohamed ‘TID’, Hamidu Salimu ‘Nyandu Tozi’, Lulu Abbas ‘Lulu Diva’, Winfrida Josephat ‘Recho’, Said Mandingo ‘Babu wa Kitaa’  na Tunda Sebastian ambao wanajihusisha na muziki wa kizazi kipya na Hamad Hashim (meneja wasanii Bongo Fleva) na Director Joan ambaye ni mfanyabiashara.

Wema Sepetu hakupandishwa mahakamani juzi. Hakimu Shaidi wa mahakama hiyo alisema kuwa kutokana na mashitaka hayo watuhumiwa wataachiwa kwa dhamana ya shilingi milioni 10 kila mmoja na  kwa kipindi cha miaka mitatu watakuwa chini ya uangalizi wa mahakama ikishirikiana na jeshi la polisi. Pia watatakiwa  kuripoti kituo cha polisi mara mbili kwa mwezi kwa ajili ya kuchunguzwa zaidi. Kwa upande wa serikali katika kesi hiyo ilisimamiwa na Wakili Nassoro Katuga huku upande wa utetezi ukiwakilishwa na Wakili Albert Sando


Loading...

Toa comment