Makonda Atoa Saa 24 kwa Wabunge ‘Wanaozurura’ Dar – Video

MKUU wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda,  leo Mei 6, 2020, ametoa Saa 24 kwa wabunge wote waliokimbia kushiriki vikao vya bunge na kwenda Dar es Salaam “kula bata” kuhakikisha wanarudi bungeni na kwamba tofauti na hapo watakamatwa kwa kosa la uzururaji kama wanavyokamatwa machangudoa wanaozurura usiku.

 

Amesema mbunge anayepaswa kuwa Dar es Salaam ni yule mwenye kibali au ruhusa ya spika wa bunge bila hivyo “ni vyema wakafunga virago vyao na kurudi bungeni ili kuepuka kukamatwa.

 

“Hakuna asiyefahamu kuwa sasa hivi tuko katika mapambano dhidi ya virusi vya corona na si uzururaji. Ifahamike huu si mji wa wazururaji,  hivyo natoa masaa 24 kwa wabunge wote kurudi Dodoma tofauti na hapo tutawakamata kwa kosa la uzururaji kama tunavyowakamata machangudoa,” alisema .

 

Aidha  amesema kwa sasa ni kipindi muhimu cha mjadala wa bajeti kuu ya serikali na wananchi waliwachagua kwenda kuwawakilisha bungeni na kupigania maslahi yao hivyo kitendo cha kukimbia vikao vya bunge ni kutowatendea haki.

 

Hata hivyo, amesema kinachomshangaza ni kuona wabunge hao wamekimbilia Dar es Salaam kufurahia maisha badala ya kwenda majimboni mwao kutembelea wananchi wanaokabiliwa na mafuriko.

 

View this post on Instagram

 

A post shared by Global Publishers (@globalpublishers) on


Toa comment