Makonda awahimiza wakuu wa idara yake kufanya kazi kwa kujituma
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda (katikati) akizungumza mbele ya wakuu wa Idara za sekta mbalimbali (hawapo pichani).
Kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni, Musa Natty, Paul Makonda na RPC wa wilaya ya Kinondoni, Camilius Wambura.
Wakuu wa idara mbalimbali wa wilaya ya Kinondoni wakifuatilia mkutano huo.
..Mkutano ukiendelea.
MKUU Wa Wiliya ya Kinondoni, Paul Makonda amewahimiza wakuu wa Idara mbalimbali kwenye wilaya yake kufanya kazi kwa kijituma na pasipo kusukumwa.
Alitoa rai hiyo wakati wa kikao chake na wakuu hao ofisini kwake, kuzungumzia utekelezaji wa mikakati ya kimaendeleo wilayani kwake.
Aliwataka kuondoa kero kwenye idara zao, kama migogoro ya ardhi na huduma mbalimbali za kijamii zikiwemo upatikanaji wa maji safi na salama.
Kuhusu rushwa, alisema anazo taarifa za baadhi ya idara kuomba rushwa ili kutoa huduma kwa wananchi, hivyo akawaonya kuwa hatawavumilia huku akilaumu utendaji hafifu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU).
Aidha Makonda amewataka maafisa Elimu wa Sekondari na Shule za Msingi wa Kinondoni kukutana Novemba 30 mwaka huu ili kujadili mipango kazi kuwawezesha wanafunzi kufanya vizuri katika masomo yao na motisha kwa walimu.
Aliwataka watendaji wote kuichukulia hotuba ya Rais Magufuli kama mwongozo wa utendaji kazi na kwamba mtendaji yeyote wa serikali atakuwa salama kama atafanya kazi kwa weledi na kuzingatia matakwa ya wananchi.
Kikao hicho kimewakutanisha baadhi ya wakuu wa idara kama, afya, Elimu, Maji, Kilimo, Mapato na Mifugo.
(NA DENIS MTTIMA/GPL)

