The House of Favourite Newspapers

MAKONDA AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA BARABARA YA AFRICANA-KINZUDI

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikata utepe kuashiria uzinduzi huo.
Zoezi likiendelea.

 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  ameweka jiwe la msingi kuashiria kuanza kwa  ujenzi wa Barabara ya Africana-Kinzudi  yenye urefu wa  Kilomita 3.3 ambayo ujenzi wake utagharimu zaidi ya Shilingi  Million 900.

 

 

Ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha  lami  inaenda sambamba na uwekaji wa matuta, mitaro ya maji, taa za barabarani, Calvert na alama za watembea kwa miguu  ambapo itajengwa na  Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA).

 

Baada ya kuzindua Barabara hiyo Makonda  amefanya mkutano wa hadhara na wakazi wa Kata za  Wazo na Mbezi Juu  uliolenga kupatia  majibu ya changamoto  zinazowakabili kwenye sekta ya Miundombinu, elimu, afya, maji, ardhi na usafiri  ambapo wakazi wa kata hizo wamefurahia kuona  kero zao za muda mrefu  zimepatiwa ufumbuzi wa haraka.

 

Katika mkutano huo Makonda  ameelezea miradi mikubwa inayotekelezwa na serikali ikiwemo ujenzi wa Reli ya kisasa  kwaajili ya usafiri wa  treni kutoka wazo kuelekea Mwenge, uwanja wa ndege  na Posta  ambayo itasaidia usafiri na kupunguza msongamano wa magari.

 

 

Makonda  amewataka wananchi waliojenga kwenye  hifadhi ya barabara  ya Afrikakana-Kinzudi kushirikiana na serikali kuhakikisha  ujenzi unafanikiwa  huku akiwataka wakazi waliojenga ndani ya hifadhi ya  bomba la maji  kutokea Ruvu kushirikiana kwa kina na  DAWASA.

 

Comments are closed.