MAKONDA AYAONYA MAKAMPUNI YA UDALALI KUTOTUMIA NGUVU

Mkutano wa  wamiliki wa makampuni ya udalali ya jijini Dar es Salaam na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda ukiendelea.

Baadhi ya wamiliki wa makampuni ya udalali ya jijini Dar es Salaam wakimsikiliza mkuu wa mkoa, Paul Makonda (hayupo pichani).

Mkuu wa  Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda  akizungumza jambo wakati alipokutana na wamiliki wa makampuni ya udalali ofisini kwake leo, Februari 13 mwaka huu.

 

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amewataka wamiliki wa makampuni ya udalali jijini Dar es Salaam, kufuata taratibu za kisheria wanapokuwa katika majukumu yao ya kikazi katika kukamata au kuondoa mali za watu wanapokuwa wakidaiwa.

 

Amewaomba pia  kuwaelimisha, badala ya kuwapiga viboko waendesha  bodaboda wanapokuwa wakitaka kuingia  maeneo ya Posta jijini Dar es Salaam.  Pia amewataka wawasilishe leo nyaraka zao za utambulisho wa kufanya kazi hizo zinazowaonyesha kuwa wao ni halali ili kuondoa makundi ya watu wanaojipenyeza na kujifanya  ndiyo wamiliki wa makampuni ya udalali.

 

NA DENIS MTIMA/GPL

 

Loading...

Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment